Download Mp3 from African

Muigizaji wa kike, Media adai kuwa yeye ndiye muigizaji bora, Chany Queen na Divine wawe makini


Hatungimana Aline wengi wanamfahamu kwajina la Media, ni muigizaji wa filamu wa Republic of Burundi Movie katika kundi la Tambwe The Great Films awali ameigiza katika filamu itwayo ZAWADI YA MWAKA akiwa kwenye kundi la The King Great Films ya mjini Bujumbura.

Mwanadada mrembo Media amedai kuwa ye ndiye muigizaji bora wa kike na amewataka wengine wawe makini kwasababu amejipanga vizuri mwaka huu na filamu nyingine itakuja kumtambulisha kimataifa zaidi.
Kampuni Tambwe The Great Films hipo kwenye maandalizi ya filamu mpya ambayo imewashirikisha ma staa kibao kama Jay Fire, Divine na Chany Queen huku katika kundi ilo kuna warembo wengi kama Media na wengine watakao itendea haki filamu hiyo.

Media amesema kuwa filamu yao mpya itakuwa ni filamu kubwa katika tasnia ya filamu. Nyota huyo katika tasnia ya filamu Tambwe The Great Films Hatungimana Aline ‘Media’ ipo tayari kuingia sokoni na kutengeneza kazi  katika viwango vya kimataifa, kazi hiyo mpya inakwenda kusaka tuzo kubwa kabisa duniani.
Back To Top