Download Mp3 from African

Mvua zilizoanza kunyesha katika Mji wa Igunga Tabora zimeanza kuleta madhara makubwa kwa wakazi

MVUA zilizoanza kunyesha katika Mji wa Igunga,Mkoani Tabora imeanza kuleta madhara makubwa kwa wakazi wa Mji huo na hivyo kusababisha zaidi ya wakazi xix wa Mitaa ya Igunga magharibi na Mtaa wa Stoo kukosa makazi ya kuishi baada ya nyumba zao kubomoka,kuanguka na kuharibu mali zao ambazo hata hivyo thamani yake bado haijajulikana.

WAKAZI hao waliokuwa wakiishi katika kaya sita,zilizopo mtaa wa Igunga magharibi na Mtaa wa Stoo,wamesema mvua hiyo iliyoanza kunyesha saa 12 jioni hadi saa moja asubuhi imewakosesha chakula wala mahali pa kuishi kutokana na nyumba na mali zao kuharibiwa na mvua kubwa kutokana na miundombinu mibovu ya mifereji ya kusafirishia maji inayosemekana ilijengwa na Wakandarasi wasiokuwa na sifa.

BAADHI ya waathirika wa tukio hilo ambao wamenusurika kupoteza maisha baada ya nyumba zao aidha kuwa na nyufa,kuta za nyumba zao kubomoka na zingine hata kuanguka,Bi,Rehema Juma amefafanua kwamba tukio hilo limetokea mwishoni mwa wili iliyopita,majira ya saa mbili usiku wakati mvua ikinyeesha ndipo maji yalianza kuingia ndani ya nyumba yake na kushindwa kutoa vyombo na kuviacha vikielea juu ya maji huku mjumbe wa nyumba kumi,Bwana Saidi Bushiri mwenye umri wa miaka 80,akilalamika kwamba mvua imesababisha nyumba yake kubomoka na kisha kukandamiza vitu mbali mbali.

KWA upande wake Diwani wa Kata ya Igunga mjini,Bwana Charles Bomani Kishepo amebainisha kwamba mvua hiyo imesababisha madhara makubwa kwani nyumba sita zimebomoka kabisa na hivyo zaidi ya watu xix kukosa makazi ya kuishi pamoja na vitu mbalimbali ambavyo thamani yake bado haijafahamika mpaka sasa

BWANA Paulo Peter Makandilo ni Mratibu wa Maafa wa wilaya ya Igunga kwa upande wake ametoa sababu zilizochangia baadhi ya nyumba zilizobomoka,ni kwamba zilikuwa zimejengwa kwa matofali ya udongo pamoja na ubovu wa miundombinu ya mitaro.
Tag : lainnya
Back To Top