Download Mp3 from African

UZINDUZI WA KAMPUNI YA KISMART ADVENT MEDIA COMPANY LTD WAFANA ARUSHA











Mkurugenzi wa Kismart Advent Media Company LTD, MERY Kismart Mollel akiwa anazungumza siku ya uzinduzi wa kampuni hiyo katika ukumbi wa ukumbi wa Asili Resort uliyopo jijini Arusha.
Na Vero Ignatus Arusha.




Meya wa Jiji la Arusha amesema kuwa ni vyema kusapoti na kuyapa ipaumbele mambo mazuri yanayofanyawa na wazawa haswa kwa uthubutu wao wa kufanya mambo ya maendeleo .

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampuni ya matangazo inayojulikana kama Kismart Advert Media Company LTD, iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Asili Resort iliopo katika Jiji la Arusha na kuhudhuriwa na wamiliki wa makampuni mbalimbali hapa nchini.

Meya huyo amewataka wananchi kuwa na tabia ya kutangaza biashara zao kwani bila kufanya hivyo hata kama bidhaa itakuwa na uzuri kiasi gani hakuna atakayefahamu thamani yake bila kuitangaza ndipo ifahamaike.

"Jengeni tabia ya kutangaza biashara zenu na bidhaa mnazokuwa nazo ndugu zangu biasahara ni matangazo msikae kimya,ukizingatia hii ni kampuni ya kitanzania,tuache kukuza vya watu tutukuze vya kwetu ndugu zangu "alisema meya.

"Mnapoona kampuni kama hii ya matangazo ndiyo fursa yenyewe hii ya kuitumia kuzitangaza biashara zenu,ukikaa kimya hakuna mtu anayeweza kuifahamu bidhaa yako au biashara yako hata kama unauza vitu vuzuri kiasi gani" alisema Meya.

Kwa pande wake mkurugenzi wa Kismart Advent Media Company LTD,bI Mary Kiamart amesema kuwa kampuni hiyo inapokea matangazo ya aina mbalimbali na kwa bei ambayo mteja atakayoimudu .

Hivyo amewataka wafanyabiashara biashara mbalimbali kutokuwa waoga kutangaza biashara zao kwani ndiyo njia pekee itakayowasaidia biashara zao kufahamika zaidi na kupata wateja zaidi.

"Msiwe waoga kuthubu kutangaza biashara zenu hapa tunasaidiana wewe unaleta tangazo nakutangazia kwa bei nzuri na wakati huohuo unapata wateja kwa upande wako ,kwa maana nyingine tunawezeshana karibuni sana. " alisisitiza bi Mary
Tag : lainnya
Back To Top