NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR, MMANGA MJENGO MJAWIRI
Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mmanga Mjengo Mjawiri, alipokua akijibu swali la
Mwakilishi wa Paje, Jaku hashim Ayoub, aliyetaka kujua sababu ya serikali kuziba madirisha katika shule hizo badala ya kuimarisha
ulinzi.
“Ni Kweli baadhi ya shule kama Nyerere, Mwanakwerekwe, Shaurimoyo, Kwatipura na nyingine, matundu ya dirisha yamezibwa kwa matofali na hivyo kupunguza upitishaji wa hewa, kupungua kwa mwaga na baadhi ya wanafunzi hupata athari ya macho na darasa kuwa na joto kali nyakati za mchana, lakini ni kwa ajili ya usalama wao,” alisema Naibu Waziri huyo.
Alisema hatua za kuzibwa kwa madundu ya madirisha ilichukuliwa na uongozi wa kamati za shule hizo kutokana na kukithiri tabia ya baadhi ya watu kuwatupia wanafunzi uchafu na vinyesi wakati wakiendelea na masomo yao.
Source: Nipashe
Tag :
lainnya