Download Mp3 from African

Je Unamfahamu Yannick d'Arc, mwanamuziki wa Enzi zile za Kiyoyo Juma, Farious, Nziza Desire na wengineo wengi?

Wengi hawamfahamu kwajili ya kuishi miaka nyingi nje ya Burundi, anaitwa Mweze Masumbuko almaarufu kama Yannick D'arc, amezaliwa Bujumbura Novemba 11, 1978, mwenyeji wa tarafani Buyenzi na Bwiza.
Ameanza kazi ya muziki mwaka wa 1990 katika kundi la dansi itwayo The Pop of Rap akiwemo Farious Big akiitwa enzi zile kwajina lake halisi Desiré. Baada ya kifo cha raisi  Melchior Ndadaye kundi ilo limevunjika.

1995, wameunda kundi nyingine la dansi na mitindo mengine itwayo Full Force Unite, pakiwemo wa nyota kadhaa kama Kiyoyo Juma mwenye makazi yake kwasasa nchini  Uholanzi na ndiye amekua kiongozi, Farious aishiye Ufaransa kwasasa, Nziza Desiré akiwa Umarekani kwasasa na wengineo wengi.

1997, Kundi la Full Force Unite ikaorodheshwa kuwania tuzo iliyo andaliwa na Studio Telaviv ya Buyenzi kwenye ukumbi wa Lycée du Lac Tanganyika, kundi la Full Force Unite imeridhika kuchukuwa nafasi ya pili baada ya kundi la Happy Children kuzawadiwa mshindi wa tuzo ilo itwayo Concour de Dance.

1998, kundi la Full Force Unite imewania tuzo nyingine iliyo andaliwa na Studio Telavivi kwa mara nyingine tena katika ukumbi wa Palais de la Nation.

1999, kundi la Full Force Unite, imealikwa kwenye Televisheni ya taifa RTNB kutambulisha wa dansi wao na vipaji na baadae wamefanya ziara yao Republic of Burundi nzima kwa kutangaza vipaji vyao (Tour du Pays).
katika mwaka huwo  mwanamuziki Yannick D'arc amejielekeza Kigali, Rwanda  na akajiunga na kundi nyingine la dansi mjini hapo itwayo  Cool Family ila ndipo hapo ameanza kuimba.

2001, Yannick D'arc amejielekeza mashariki ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Goma na Bukavu pia Uvira kwa tamasha mbali mbali akiwa pamoja na rakiki yake AC. Mwaka huwo huwo amerudi tena Burundi  na akajielekeza tena Rwanda kwa uzinduzi wa Centre Culturel Francais mjini Kigali akishirikiana na Nziza Desire, Dr Claude na CMJ. Hapa ndipo ameanza kujulikana na wakafanikiwa kupata ajira za hapo mjini kigali.

2004, amerejea nchini mwake Burundi, kwa kurikodi nyimbo yake ya kwanza katika Studio maarufu enzi zile itwayo Kukirimba Art, chini ya mikono yake Producer Romeo wa Kundi la Etoile du Centre, nyimbo itwayo Saga Africa iliyo shamiri mpaka mwaka 2005. Kupitia nyimbo yake hiyo ameitwa nchini Rwanda kwenye tamasha ya kumpokea Miss 2000 wa Ufaransa aitwaye Sonia Rolland. Baada ya kukamilisha aliko yake amerudi tena Republic of Burundi kurikodi nyimbo nyingine ya pili   itwayo Ton Attitude akishirikiana na Rui Dog.

2006, Yannick D'arc amejielekeza Kampala  na akafanikiwa kurikodi nyimbo kadha uko kama C'est comme ca la vie na zingine. Mwaka huwo huwo  amesafiri kwenda Umarekani na ndipo amerudi nakuzamia nchini Kenya  kwa tamasha mbali mbali na kufanikiwa kurikodi nyimbo nyingi akishirikiana na wasanii wa nchini hapo.
Kwasasa yupo Studio na ameachia nyimbo yake mpya ambayo mwanamuziki mrundi  maarufu duniani Nimbona Jean Pierre alias Kidumu ameipongeza sana.

Mishe Mishe Media ipo kwajili ya kukuza muziki na mambo mengi hapa duniani ndio sababu tumejaribu kuwasogezeeni nyimbo yake hii mpya ya mwanamuziki kongwe kwenye game hii ya muziki ambaye kwasasa nchini Republic of Burundi nikama wameisahau jina lake na kazi zake ila ugenini anashamiri kiasi kikubwa.

Inaitwa Girl of my Destiny  ya kwake Yannick D'arc mwenye makazi yake Nairobi Kenya, nyimbo ipo chini ya mikono ya producer mahiri MG Dungeon.


Endapo utapendelea kazi zako zipatikane kwenye tovuti yetu hii, unaweza wasiliana nasi kwenye namba +257 75707305
Back To Top