Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, Natty E, Msafiri alisema kikubwa na muhimu ni kutafuta exposure katika kazi zao. Anadai akienda huko hukutana na watu ambao hajawazoea na kutengeneza connectedness muhimu huku pia akijifunza njia tofauti za kufanya muziki.
Amesema sababu nyingine ni upatikanaji rahisi wa location, models na vitu vingine muhimu kuliko ambavyo kwa Tanzania vina mlolongo mrefu. Amesema kama unataka kutumia kitu au sehemu ya kawaida tu kwenye video, itakulazimu kuzunguka BASATA, bodi ya filamu na mamlaka zingine ili kupewa kibali.
Ameongeza kuwa kwa Afrika Kusini kama msanii anataka kutumia nguo za polisi huandika barua moja tu na hujibiwa siku hiyo hiyo na kuanza kazi. Msikilize hapo chini.
Tag :
lainnya