Mchezaji wa timu taifa Intamba murugamba pia wa klabu Bidvest Wits ya nchini Afrika Kusini, Papy Faty amefunguka kuhusu hatma ya kujiunga na klabu nyingine ambayo amekataa kuitaja jina na kusema kuwa kadiri ya siku inavyo kwenda, ataweka adharani mambo yake.
Akizungumza na muandishi wa Mishe Mishe pia na Mtangazaji wa kituo cha Radio Culture, kwenye mazoezi ya timu ya taifa Papy Faty ameongelea hatma ya uhamisho wake na pia kuhusu mechi ya mwisho dhidi ya Niger ya kuwania tiketi ya kufuzu kombe la Can2017 ambapo tunatambua vyema nchi ya Republic of Burundi imekwisha aga mashindano na kinacho salia ni kutopteza nafasi nzuri ya orodha ya FIFA inayo tolewa mwezi baada ya mwezi.
"unaona tunavyo endelea na mazoezi na pia kuna vijana wapya kama wawili na ninaimani tutafaulu kupata ushindi nchini Niger na pia kuhusu hatma yangu msimu huu ni kwamba director wangu anazidi kuendelea na mazungumzo na klabu yangu Bidvest Wits na pia kuna klabu moja inanihitaji siwezi kuitaja jina kwasasa ila itajulikana tu mambo ya uhamisho wangu ikikamilika", amesema Kiungo mahiri wa timu ya taifa Intamba Murugamba, Papy Faty.
Tusubiri tuone kabla ya dirisha kubwa ya usajili haijafungwa ifikapo mwisho wa mwezi huu saa sita usiku, ndipo tutajua klabu mpya ya Papy Faty ao pengine akasalia katika klabu yake Bidvest Wits.