Mchezaji kiungo wa timu ya taifa ya DR Congo pia wa klabu ya FC Metz, Yeni Atito N’Gbakoto amesaini mkataba wa misimu mitatu na Queens Park Rangers ya Uingereza (daraja ya pili) kwa mujibu wa tovuti rasmi ya klabu hiyo ya Uingereza.
Mchezaji huyo mweye umri wa miaka 24, N'Gbakoto ameachana na klabu yake ya kwanza na ameibuka kama mchezaji bora wa klabu yake ya daraja ya pili nchini Ufaransa kwa jumla amemaliza msimu na mabao 12 na kutoa pasi xi katika mechi 38.
Aidha , N'Gbakoto bado kijana na ana umri mdogo wangeweza hivi karibuni kumuweka katika mstari wa mbele wa timu ya taifa DR Congo. Hakika kocha mkuu wa DR Congo Florent Ibenge amesema hivi karibuni anatarajia kuchukuwa uwezekano wa kumuanzisha kijana huyu kwenye mechi yake ya kwanza akivaa jezi yenye rangi ya nchi yake kwa awamu ya kufuzu kombe la Dunia 2018.