Mwanamuziki maarufu Afrika Mashariki kutoka Burundi, Niyonzima Nassor Salum kwajina maarufu Lolilo Mzizi wa Jiwe ao Lizzo.com, amefunguka kuhusu tabia chafu inayo zidi kuharifiwa kwenye vituo vya radio nchini Burundi.
Media zinauwezo mkubwa wakuifanya muziki upendwe mahali pote ila tofauti na media za nchini Burundi.
kwa madai ya Lolilo ameiambia Mishe Mishe kuwa media za Republic of Burundi zinatabia mbaya ya kupenda kazi za nje kuliko kupenda za kwao.
Radio nyingi za Republic of Burundi zinapitisha nyimbo za nje sana kuliko kuthamini za nchini mwao, mpaka mwanamuziki Lolilo amefikia kusema kuwa jambo ilo inauma sana na sio poa kama wanamuziki wa nje wanatowa pesa ili nyimbo zao zipitishwe basi waseme ili wanamuziki wa Republic of Burundi Flava waanze kuwapa pesa ilimradi nyimbo zao zipitishwe.
Lolilo ameamua kutema na kusema yalio moyoni kuusu Media za Republic of Burundi nakusema
"ndugu zangu na marafiki wote ambao munaopenda Republic of Burundi Flava, kuna jambo imeniuma sana leo naamua kuisema kweli. Radio zetu (Burundi) zinaipa nafasi kubwa nyimbo za nje kuliko za nyumbani, kwanini wanapenda kupitisha nyimbo za nje kuliko kuthamini za nyumbani? tizama kama TV Salama nina saa nzima niko naifatilia wanaipitisha nyimbo ya Alikiba (Tanzania) mara sita ila hata nyimbo moja ya msanii kutoka Republic of Burundi sijaona. kama wanawapatiaga pesa hao wasanii wa nje tuambieni nasi tuwe nawapa pesa ili muziki wa Republic of Burundi Flava ufike mbali. Media za Republic of Burundi badilikeni na warundi wote tubadilike, haipendezi na sio fresh", amesisitiza Mzizi wa Jiwe Lolilo.