Mtangazaji Ismail na Msani Lolilo |
Baada ya msanii Niyonzima Nassor Salum almarufu kama Lolilo Lizzo.com ao Mzizi wa Jiwe kutangaza malalamiko yake kuwa media za Republic of Burundi azichangii kwenye Republic of Burundi Flava. Lolilo amedai kuwa nyimbo ao video zao hazipitishwi kwenye vituo vya radio na TV uku akitaja badhi ya Media kama Rema FM na TV Salama kuwa zinapenda kupitisha kazi za nje kuliko za nyumbani (Burundi).
Mtangazaji wa Radio Rema FM ajulikanaye kwajina la Ismail Niyonkuru, amesikika kwenye kipindi chake na kuwaomba wanamuziki wote ambao wanadai kuwa kazi zao hazipewi nafasi kwenye Media waje pekee yao kwenye radio awaambie tatizo ya nyimbo zao kutopitishwa kwenye runinga za Media. Mtangazaji huyo ameongeza na kusema kuwa kuna wanamuziki wanadai kuwa hawapewi nafasi ukiwachunguza hawana akaunti ya youtube ikimaanisha kuwa bado hawajuwi wanacho kifanya katika ulimwengu wa muziki na wengine video zao hazina madili ya kuridhisha uku wakionesha mambo isiyo endana na mashahiri ya nyimbo zao.
Ismail ameongeza na kumtaja Msanii Lolilo kuwa ni msanii kongwe ila bado angali na akili ya ki
local (kitoto) kwasababu tangu haanziye kazi ya muziki, hajawahi kuwa na akaunti ya youtube. Msanii kukosa akaunti yoyote ya kutangaza kazi zake binafsi ni jambo la kushangaza ukichunguza utakuka msanii kongwe hakose vifaa vitakavyo mutambulisha kimataifa na kutowasumbuwa wale ambao wanao fatilia kazi zake.