Download Mp3 from African

Ndayishimiye Dumu anatarajia kujiunga na Foresters FC ya Republic of Seychelles Ivi karibuni

Mshambuliaji kutoka Burundi, Ndayishimiye Dumu amejielekeza siku ya Ijumaa jioni nchini  Republic of Seychelles kwa kukamilisha usajili wake kwa kujiunga na Foresters FC. 
Ijumaa jioni Mchezaji mrundi Dumu amekuwa Bujumbura  kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa na kuelekea  Republic of Seychelles kukamilisha hoja ya kujiunga na  Foresters Mont Fleuri Football Club.

Dumu mwenye umri wa miaka 29, mchezaji wa zamani wa Flambeaux de l'Est ya Mkoani Ruyigi msimu uliyo pita, alithibitisha kuifungia mabao sita kwenye hatua ya marudiano ya Ligii Kuu, uku akiisaidia klabu kuto shuka daraja.

Ndayishimiye Dumu amesajiliwa na klabu ya Flambeau de L'est ya Mkoani Ruyigi katika dirisha dogo la usajili akitokea Republic of Kenya katika klabu Kitengela Shooters kwenye Super League.

Dumu aliahidi timu yake mpya hiyo kuwa watarajie mambo makubwa kutoka kwake uku klabu yake mpya imekuwa miongoni mwa timu 12 bora ya Ligi Kuu nchini Seychelles

"Nina furaha sana. Nataka kuiambia timu yangu mpya Foresters na mashabiki  mashabiki kutarajia mambo mema kutoka kwangu. Nami nitaitumikia klabu hii kwa moyo wangu wote na nguvu zangu zote". amesema Dumu.

Kila la kheri Ndayishimiye Dumu katika Klabu yako hiyo mpya. 
 
Back To Top