Mwili wa Michael Juma mwenye umri wa miaka miwili na nusu ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) kaburi lake lililazimika kufukuliwa kwa ulinzi wa jeshi la polisi ili mwili ufanyiwe uchunguzi kutokana na kuibuka maneno yenye kutatanisha wakati alipokuwa akiugua alivuja damu nyingi puani na kuvimba mwili.
Tukio la kufukua kaburi hilo ambalo mwili wa marehemu mtoto huyo alikuwa amezikwa tangu siku ya Jumapili pembeni ya nyumba waliyokuwa wakiishi na wazazi wake limetokea juzi siku ya alhamisi katika kijiji cha Bunambiyu halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga nakuwashangaza wakazi wa eneo hilo.
Katibu wa chama cha albino (Tas) mkoani Shinyanga Lazaro Anael alisema kuwa kitendo cha kuufukua mwili kimewashangaza tangu alipopata taarifa kuwa kifo cha mtoto huyo kumezuka maneno kuwa kina utata wakati yeye alishiriki mazishi
Naye diwani wa kata ya Bunambiyu Richard Sangisangi aliyekuwa amekataa mwili huo kufukuliwa nakugoma kuwaita majirani kwaajili ya kufukua mwili.
Tag :
lainnya