Download Mp3 from African

TV mpya ya Majay kuingia DSTV moja kwa moja

Kituo kipya cha runinga kinachomilikiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa EFM, Dj Majay kitaanza kuonekana hivi karibuni kupitia DSTV.
Kituo
Tayari kituo hicho kimekamilika kila kitu huku kikisubiriwa kuanza kuonekana siku si nyingi zijazo. Majay amekuwa akitease kwenye Instagram kwa muda sasa kuhusu kituo hicho cha TV ambacho bado hajasema kitaitwaje ingawa awali kuna taarifa kuwa kinaitwa Target.
Kituo
Ameweka teaser inayoonesha kuwa tayari wameingia mkataba na DSTV kuanza kuonekana kwa kituo hicho kipya.
Ujio wa TV hiyo unaongeza himaya nyingine kwa Majay ambaye tayari kituo chake cha redio, EFM ni miongoni mwa redio zenye wasikilizaji wengi huku ikiingia mkwanja mrefu kupitia matangazo kibao.
Hata hivyo biashara ya TV si ngeni kwa Majay. Miaka kadhaa iliyopita kampuni yake ilikikodisha kituo cha runinga cha DTV na kukifanya kuwa moja ya vituo vya runinga vya burudani vilivyokuwa na watazamaji wengi.
Tag : lainnya
Back To Top