Msanii wa hip hop Tanzania,Stereo amedai kuwa wanamuziki wengi wa hip hip hawakubaliki kwenye jamii kutokana na mionekano yao na kutokuwa na nidhamu katika kazi.
Akiongea kwenye kipindi cha Ladha 360 cha EFM ,msanii huyo amedai matumizi ya lugha za kihuni na matusi kwenye nyimbo zao kunafanya watu wenye staha kutosikiliza muziki huo.
“Mimi nawashangaa wasanii wengi wa hip hop ,kwani mpaka utukane ndio uonekane unachana sana?!..jinsi tunavyoonekana pia ,utakuta mahereni ,micheni,mabuti makubwa ,vitu kama hivyo vinawatisha wazazi, hata mama yangu aliwahi kuhoji vitu kama hivyo.Wasanii wengi hawajui waseme nini ili watu fulani wenye akili zao wawasikilize,washua hawawezi kukusilikiza kama unachana matusi” alifunguka Stereo ambaye aliwataka wasanii wa hip hop kuwekeza kwenye mionekano ambayo ina tija kwenye jamii.
Tag :
lainnya