Download Mp3 from African

Roma na Dayna Nyange wamewahi kuwa wapenzi ? Roma amefunguka haya..

Msanii wa Hip Hop Tanzania,Roma amefunguka kuhusu tetesi za yeye kuwahi kutoka kimapenzi na msanii wa kike Dayna Nyange baada ya wawili hao kuonekana kuwa karibu sana.
Akijibu tuhuma hizo kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa radio ,Roma amedai kuwa anamchukulia Dayna kama mdogo wake ambaye yuko naye karibu na hakuna mambo mengine yanayoendelea kati yao.
Dayna ni mshikaji wangu,yaani kama mdogo wangu,niko nae karibu sana ndio maaana hata kwenye harusi yangu alikuwa anacheza sana..sema ndio hivyo ukishakuwa karibu na mtu fununu zinakuwa nyingi,achana na hizo fununu“alisema Roma ambaye aliingia rasmi kwenye ndoa miezi kadhaa iliyopita.
Tag : lainnya
Back To Top