Waswahili husema ulimi hauna mfupa ni pale mtu anapokua anakosea kutamka neno, au kutamka neno ambalo hakulimanisha wakati hule, Mwanamuziki wa taarabu mwenye makazi yake nchini Tanzania akiwa mwenyekiti wa kundi la Umoja Band, Abduly Misambano ametamka neno mbele ya watangazaji wa habari akifunguka kuhusu ujio wake nchini Burundi.
Msemo huu umemkuta Mwanamuziki huyo pale ambapo akiwa akiongelea mipango mingi kuhusu muziki wake na albamu mpya ya kundi Umoja Band ambayo inatarajia kuachia wimbo wa amani.
Mwanamuziki huyo amejikuta akitoboa siri ya kundi kwa kusema kwamba
Tumefikia kuunda kundi moja ya Umoja Band na kwasasa nimerudi Republic of Burundi na mwenzangu Athumani kwa kukamilisha kurikodi nyimbo kadhaa zitakazo wakilisha albamu yetu mpya, pia katika uzinduzi wa Albamu hiyo tutamuleta mwanamama Adija Kopa wa Tanazania.
Baada ya kutamka neno kwamba Adija Kopa atakuwepo kwenye uzinduzi wa albam hiyo, Misambano ameongeza na kusema kuwa
sikupendelea kuongelea leo ujio wa Adidja Kopa nchini Republic of Burundi katika siku ya uzinduzi wa albamu yetu ila basi ulimi hauna mfupa, tambueni kuwa ukweli ndio huwo.