Mwanamuziki Abduly Misambano anaefanya vizuri sana kwenye tasnia ya muziki wa Taarabu ataka kurudisha changamoto kwa jamii yake hasa kule alipokulia enzi za udogo wake.
Nyota huyo anatarajia kufanya hivyo kwa kutoa burudani mbali mbali ikiwemo kurikodi nyimbo nzuri, tamasha za mjini na mkoani pia na kutengenezesha t-shirt za kundi.
Muziki wa taarabu ina historia ndefu katika muziki wa Republic of Burundi kama ulivyokuwa muziki wa dansi. Wapenzi wa taarabu waliiweka taarabu katika vyanzo kama taarabu ya Buyenzi, taarabu ya Rumonge, taarabu ya Gitega, taaarabu ya Ngozi na maeneo yote wanaozungumza kishwahili.
Katika anga za leo kuna vikundi vingi vinavyotangaza vinapiga muziki wa taarabu, na wengine wakisema kuwa kinachopigwa pigwa sasa si taarabu, hakina uhusiano wowote na taarab!
Lakini Misambano alijibu madai hayo na kusema kuwa hiyo ni kawaida katika anga za muziki, jambo ambalo halina ubishi muziki hukuwa na kubadilika kutokana na mambo mengi ikiwemo teknolojia, na muingiliano wa tamaduni nyingine.
Muziki wa taarabu nchini Republic of Burundi umedidimia kiasi kikubwa sana, ndio sababu ya nyota huyu akishirikiana na wengine kufikia kuunda kundi moja kwa lengo ya kurudisha hadhi ya taarabu nchini Burundi.
Mwanamuziki huyo alisema anakuja kwa malengo ya kurudisha heshima na hadhi yake kama ilivyokuwa hapo awali na kurudisha heshima ya muziki wa taarabu nchini.