
DAR ES SALAAM: Kufuatia msala wa kutuhumiwa kujihusisha na utumiaji au biashara ya madawa ya kulevya unaosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, sasa baadhi ya mastaa wanadaiwa kukauka kwenye viwanja vya starehe.
Chanzo makini ambacho ni mmoja wa mastaa, alifunguka kuwa tangu sakata la kutajwa majina lilipoanza hali ni mbaya kwa mastaa hasa wa kike kwani waliokuwa wakiwapa fedha za kufanya mbwembwe mjini wengi wanahofia kutajwa huku wengine wakiwa wametajwa tayari.
“Ukweli hali ni mbaya kwa sisi mastaa ndiyo maana unaona hata zile mbwembwe za mjini hazipo tena, wengi tunahofia kutajwa huku wengine wakiwa wametajwa au wadhamini wao.
“Wasanii wa kike ndiyo wenye hali mbaya zaidi kwani wale mapedeshee waliokuwa wakiwapa jeuri wamepunguza kuwapa fedha huku wengine wakiwa wameshatajwa majina hali ambayo inaendelea kuzua hofu zaidi,” kilisema chanzo hicho.
Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa, ni kweli hali ni mbaya kwa mastaa na wengi wao wakiwa na hofu kubwa baada ya kuona wenzao au watu wao wa karibu, wametajwa kwani hata wakipigiwa simu zao za mikononi wana hofu kuzipokea au hata wanapofuatwa majumbani mwao husemekana wamesafiri.
Uchunguzi huo ulibaini kuwa, kwenye kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar, hivi sasa pamekauka kwani wahudhuriaji ni wachache huku mastaa wakiwa hawaonekani kama ilivyokuwa zamani walipokuwa wakijirusha.
Tag :
lainnya