
Muziki unasafirika umbali usioweza kuufikiria. Na katika nyakati hizi za mchipuko mkubwa wa mitandao ya kijamii, kasi yake ni ya kutisha. Lakini cha kupendeza zaidi, ni kuwa muziki huongea lugha ya dunia. Waweza kuupenda wimbo usiouelewa hata neno moja, lakini sauti na ala zake zikakufanya uusikilize bila kuuchoka. Lakini ni muziki uliotungwa kwa umaridhawa mkubwa unaoweza kukidhi viwango hivyo.
Video hii ilioongozwa na Director wa KWETU STUDIO Tanzania, na Audio ipo chini ya Producer Lizer Classic wa Wasafi Records imejijengea headlines nyingi kwenye Runinga ,Radio ,Blog tofauti barani Afrika.
Kebby boy pia amekuwa Nominated katika Tuzo za JAIYE AFROMUSIC nchini Nigeria katika kipengele cha BEST AFROMUSIC na kwasasa imezijenga TOP 10 za Mzansi four Show ''SABC1' nchini South Africa.
Inashangaza mno katika umri huu mdogo kimuziki alionao kuweza kutengeneza kishindo kinachozifikia hata nchi zenye watu wasioelewa hata neno moja la Kiswahili. Sijawahi kuona video yenye maoni chanya kwa zaidi ya asilimia zaidi 95 huku wachangiaji wengi wakiwa si Waburundi kama kwenye video ya kijana huyu. Nenda kajionee mwenyewe na utaamini utabiri wangu kuwa, Kebby ni kitu kikubwa cha baadaye Afrika.
Kama bado hujaiona ''SINA LAWAMA'' ya Kebby Boy hii apa chini....