Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limekamata shehena kubwa ya dawa za kulevya na kumfukuza kazi askari mmoja wa kituo cha polisi cha wilaya ya Kishapu kwa kosa ka utovu wa nidhamu na kukosa uadilifu kazini pamoja na kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amesema Jeshi hilo limefanya oparesheni ya kimya kimya kwa muda wa wiki mbili mfululizo na kufanikiwa kuwakamata watu 33 wanaotuhumiwa kujihusisha na usafirishaji na uuzaji wa dawa za kulevya huku likikamata shehena kubwa ya dawa za kulevya.
Aidha Kamanda Muliro amesema katika oparesheni hiyo amekamatwa mtu mmoja mwenye uraia wa Tanzania na Mascat Sultanate of Oman ajulikanaye kwa jina la Saidi Nasoro miaka 27 mkazi wa Nyasubi Kahama kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji na uuzaji wa dawa aina ya heroine huku akimtaja Ashura Ramadhani miaka 38 kwa tuhuma za kuendeleza biashara ya mume wake ambaye amefungwa kwa makosa ya usafirishaji na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Kwa wakati huo huo Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limelazimika kumfukuza kazi askari wake namba F.9899 PC Hasan Kavindi kwa kukosa uadilifu wakati huu wa vita dhidi ya dawa za kulevya na kulisaliti jeshi la polisi kwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Tag :
lainnya