Mwana mama Terresa Nealy akiwa kama meneja wa msanii wa muziki wa Burundifleva King Moses mwenye makazi yake nchini marekani, alipokelewa kwa masham sham na mashabiki wa mwanamuziki huyo kwenye uwanja wa ndege ya jijini Bujumbura akitokea Marekani.
Mwana mama huyo alifurahishwa na mapokezi ya mashabiki wa msanii wake na kusema kwamba hakuwa anategemea kama King Moses anapendwa sana nchini Republic of Burundi na pia anaamini kuwa siku za mbele msanii wake King moses anaweza kuchafua anga la muziki kwa utunzi wake na uimbaji wake.
Warundi wenye moyo wa upendo na uzalendo pamoja na Watangazi wa habari walijitokeza katika uwanja wa ndege kumpokea mwana mama huyo wakiwa na mabango kabisa yenye maneno ya kumsifia King Moses kwa kuipeperusha vyema bendera ya Republic of Burundi katika muziki.Uwanja wa ndege uligubikwa na kelele za furaha na sauti zilisikika zikitaja jina la King Moses.
Mwana mama Terresa Nealy baada ya kufika aliwashukuru sana waliofika kumpokea na kusema safari yake ilikua nzuri na amejifunza kuwa nchi ya Republic of Burundi ni nchi ya amani na upendo tofauti na jinsi wanavyofikiria wakiwa nje ya nchi. Kwa upande mwingine alitoa shukran za dhati kwa watangazaji na kusema bila wao King Moses hatafika popote katika muziki, inabidi media zi sapoti muziki wao kwasababu wanaweza huku akimaliza nakusema ''Ndanezerewe cane kandi ndabakunda''.