Download Mp3 from African

Napenda Kusaidia watu kuliko Starehe _Natacha La Namba

Mwanamuziki maarufu nchini Burundi, Natacha amesema anapenda kusaidia watu sana kuliko starehe na anapatwa na uzuni moyoni akiona mwana mama hajiwezi kimaisha, aliyasema hayo baada ya kumaliza kutoa zawadi mbali mbali  kwa wakina mama tarafani kinama tarehe 09 Machi, 2017.

Mwana mama mrembo Natacha alisema katika maojiano na waandishi wa habari kuwa anaposaidia wa mama hukumbuka namna gani aliwahi kusaidiwa na kulelewa na wa mama tofauti pindi alipokua mtoto mtahani hapo. Aliongeza kwamba maisha yake kabla ya kufikia umri  na mafanikio aliyonayo sasa, nikutoka kwa mapenzi ya wakina mama na alisaidiwa sana na watu.
''Fikra hii imenikujia ghafla tu na nikaamua kubisha hodi mahali pote ili wanisaidie nifanikishe mpango huu, kuna sehemu wamenisikiliza na wakakubali kunisaidia ili niakikishe katika sikukuu ya leo wa kina mama wafurahi kama wengine. Maumivu ya shida na uhitaji nayafahamu, ndio maana najituma kwa kusapoti wengine, najikumbusha nilivyokuwa nahitaji msaada na bila shaka wana mama hawa wamenipa kadri ya uwezo wao nami leo sina budi ya kuwapongeza na kusema asante sana wa mama wote.

Najuakuna wengine wamekosa zawadi ila siku hazingadi ipo siku nitachukua mdaa wakubisha hodi mahali pote ili tuakikishe tunawasaidia wote. Tena nampongeza sana Kiongozi wa kinama mwenye busara, nilikaa naye kwa mda mfupi, lakini nilichojifunza kutoka kwake ni kama nime kaa naye mwaka mzima, napenda uongozi wa mwanamke sana huwa unamaendelea na amani''. Alisema Natacha La Namba.
Back To Top