UMOJA BAND ni muungano wa wanamauziki wa mwambao au Taarabu nchini Republic of Burundi yenye makazi yake Nchini Tanzania, ikiundwa na Niyonzima Omary ambae ni Meneja na akiwa msemaji wa kundi pamoja na Abduly Misambano ambae ni mwenyekiti wa Kundi hilo.
Hatimaye mwanamuziki wa Taarabu maarufu Afrika Mashariki, Abdully Misambano anatarajiwa kuwasili Republic of Burundi akiwa pamoja na Athumani Kilanga, Jumapili hii.
Wanamuziki hawo wa Taarabu wanakuja na niya ya kurikodi nyimbo 10 ambazo zina malengo ya kuhudumisha na kuhimarisha amani na upendo nchini Burundi.
Abduly Misambano anakuja kwa malengo ya kurudisha heshima na hadhi yake kama ilivyokuwa hapo awali na kurudisha heshima ya muziki wa taarabu nchini.
Aidha, ujio na arakati nzima ya kundi Umoja Band inaendelea kudhaminiwa na Omary Niyonzima ambae anazidi kujitolea kadri ya uwezo wake kuwezesha mpango huwo ikiwemo kutengeneza T-shirt za kundi.
