Na.Vero Ignatus Arusha.
Wito umetolewa kwa watanzania watumie vipaji walivyonavyo ili kuijenga Tanzania yenye Amani na upendo bila kujali itikadi za dini wala vyama huku wakijuaya kwamba watu wote wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.
Hayo yamesemwa na muanzilishi na mkurugenzi wa The worshiperz Abednego Peter Hango katika hafla ya kumshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea iliyofanyika katika ukumbi wa New Safari Hotel jijini hapa .
Hango amesema kuwa wameamua kiufanya hafla hiyo kwani yapo mambo mengi ambayo Mungu amewatendea siyo tu kwa mwaka huu wa 2016 ila tangia kuanzishwa kw kundi hilo mwaka 2008 ,wakiwa na malengo ya kuwaleta vijana pamoja wenye shauku ya kumtumikia Mungu,ambapo hadi sasa waapo waimbaji 36 .
Amesema kuwa maono ya kundi hilo ni kuwafundisha na kuwaleavijana pamoja na waimbaji kwa ujumla ili wawe waabuduo halisi na wahudumu na siyo kuwa waimbaji pekee jambo ambalo wamefaulu .
Wakati huohuo Kundi The worshiperz wameandaa tamasha kwakushirikiana na kundi la Gospel Kitaa linalofahamika kama Sifa za Yeriko litakalofanyika hivi karibuni katika Newlife City Church lililopo mkoani hapa tarehe 9.12.2016.
Tamasha hilo litawashirikisha waimbaji kutoka nchini Afrika ya kusini,akiwemo Mercy Manqele kutoka kundi la Joyouus Celebration,Spokazi Nzumalo kutoka kundi la Soweto Gospel Kwaya pamoja na Kgotso Makgalema kutoka kundi la Spirit of Praise.
Aidha ameainisha waimbaji wakataokuwepo kutoka jijini hapa ni pamoja na Pcasf,Cahogos,Machalii wa Yesu ,Voice of Joy,na Yusuph Nahashon
Tag :
lainnya