![]() |
Tigana |
Kocha Kirumba-Karumba Tigana kutoka Republic of Burundi ameachishwa kazi kama kocha mkuu wa timu OC. Muungano ya Bukavu, DR Congo.
Kocha Tigana alijiunga na klabu hiyo msimu huu ameachishwa kazi baada ya kuandikisha matokeo duni.
Kocha Tigana ameshinda michezo miwili tu katika michezo nne kwenye kikosi hicho cha OC. Muungano ya DR Congo, baada ya kupoteza dhidi ya Daupin (1-0) na Bukavu Dawa (0-1) amepewa kibarua ghafla ya kuachishwa kazi kama kocha mkuu wa timu hiyo.
Mashabiki na wapenzi wa timu OC. Muungano wameshangazwa na hatua hii ya kumuondowa kighafla kocha Tigana baada tu ya kupoteza michezo miwili huku akifanikisha kuipandisha timu nafasi ya nne kwenye msimamo wa mda wa ligi kuu ya DR Congo.
![]() |
Kocha Jeannot |
Bila shaka timu hii imekwisha mpata kocha mwingine na nafasi ya Tigana imenyakuliwa na Kocha Witakenge Jeannot mwenye asili ya DR Congo ila kaichezea timu ya taifa ya Rwanda, mchezaji wa zamani wa APR, Rayon Sport za Rwanda, Lupopo ya DR Congo, Maniema Fantastique, Inter Star za Republic of Burundi pia Oc. Muungano.
Jeannot Witakenge ameteuliwa kama kocha mkuu wa klabu hiyo baada ya kuachishwa kazi kocha Tigana, ata hivyo timu hii kwasasa wanamtafuta sana kocha Vivier Bahati wa Musongati ( Burundi) aliyewayi kuwa kocha wa timu hii huku wakimuomba arudi asaidizane na kocha mpya.