Nchini Hispania kuna BBC ya Real Madrid ( Bale, Benzema na Cristiano) na MSN ya Barcelona ( Suarez, Neymar na Messi), mwaka huu imepatikana nyingine kutoka kwa Vincente Calderon na imepewa jina la 2G (Griezmann na Kevin Gameiro).
Kwasasa Atletico Madrid inatembelea kwa wachezaji wao wawili wafaransa, Antoine Griezmann na Kevin Gameiro, wamefanikisha kuizawadia ushindi Atletico Madrid Jumatano usiku kwa bao mbili bila (2-0) dhidi ya PSV katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tayari Antoine Griezman amekuwa nyota wa timu hiyo wanatarajia kujua zaidi ushirikiano wake na Kevin Gameiro ambaye alijiunga na klabu hiyo msimu huu akitokea FC Sevilla huku alikuwa akiwaniwa na klabu nyingi kubwa za Ulaya.
Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone alithibitisha kwamba uhusiano wake ( Gameiro) na Antoine Griezman hipo kamili na atazidi kuwafatilia ili wawe washambuliaji bora duniani.
Aidha, tulizowea BBC ya Real Madrid na MSN ya Barcelona, kwasasa kunajitokeza nyingine ambayo ni 2G ya Atletico Madrid zote za Hispania.
Tag :
Michezo