Msanii wa Republic of Burundi Fleva, Akes Don anajivunia kumaliza arakati yote ya shooting ya video ya wimbo wake mpya aliyoshirikiana na Happy Famba aliyoipa jina la ''Kizunguzungu''.
Hakuficha hisia zake na kuonesha kiasi gani anawapenda mashabiki zake kwasababu amegundua ni kiasi gani walivyokubali wimbo wake na ndio sababu ya kukamilisha video ya wimbo huwo huku akiwa hana shaka kuwa video ya wimbo Kizunguzungu haitakumbwa na mikosi.
Video ya wimbo ''Kizunguzungu'' imepangwa kutoka rasmi March, 04, 2017, sherehe za uzinduzi wa video hiyo zitafanyika Kinama kwenye ukumbi wa Treibeka Hill Top Ten majira ya usiku na kiingilio ni pesa elfu mbili (2000fbu).
Tuakumbushe kuwa Akes Don ameshatuonesha kipaji kingine cha kuongoza utengenezaji wa video za muziki, ndio maana watu wameanza kukaa mkao wa kula kusubiria ujio wa video hiyo.