Serikali imesema kitendo cha baadhi ya wizara kuhamia Dodoma na kutumia majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), hakumaanishi kwamba hakuna majengo, bali ni kutumia majengo ambayo yalikuwa hayatumiki chuoni hapo.
Kauli hiyo imetolewa bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akitoa ufafanuzi kuhusu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo aliyeshangaa wizara kutumia majengo ya Udom, akadai ni kuchanganya wizara na elimu.
“Mpango wa kuhamia Dodoma na kutumia majengo ya Udom, ni utaratibu wa kawaida wala hauna lengo la kuvuruga masomo au kuingiliana na wizara na taaluma chuoni hapo, isipokuwa ni kutokana na Udom kuwa na majengo mengi ambayo yalikuwa hayatumiki, majengo hayo yatatumika na baadhi ya wizara, lakini shughuli zake hazitaingiliana na shughuli za elimu zinazotolewa chuoni hapo. Udom ilianzishwa kutokana na nia ya CCM kwa lengo la kupanua elimu kuwafikia Watanzania wengi, lakini majengo mengi yamebaki bila kutumika hivyo, wizara kuyatumia katika kipindi hiki si vibaya,” amesema.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya awali alisema kitendo cha wizara kutumia majengo ya Udom ni kitendo cha muda mfupi, wakati serikali ikijipanga ili kila wizara kuwa na majengo yake.

Tag :
lainnya