Kwasasa homa la bifu inazidi kuwa hatari nchini Republic of Burundi mpaka baadhi ya wasanii wameamua kupenya kupitia bifu zisizo wausu.
Hizi vita za katika sanaa ni bifu za kijinga sana, hazileti maendeleo bali chuki tu, vitaa kati ya wasanii sio jambo la kushangilia hata kidogo, kwani mtu akihisi kama wamemlenga kwenye nyimbo, kujibu ya nini? na kama ukijibu matusi adharani kwenye wimbo wako ya nini? nawe unachukuwa mda kuingia kwenye mambo ya sio kuhusu kwanini? kama ulikua na bifu na mwenzio tangu kitambo kwanini uyazungumzie leo?
Bifu inatuma mnapoteza urafiki kwa umaarufu wa siku mbili, walio fanya bifu nchini leo wapo wapi? Wanajeshi na Wakali Power, Lolilo na Fizzo, Fizzo na Uncle Crazy, T Max na Dirop, ukiwaangalia hawa wasanii wote ni wakali ila ujinga ndio umesababisha kupoteza mda wao na kutengeneza nyimbo zisizokua na maendeleo mpaka kwasasa hawana hata tuzo la bifu, kama wangelitumia mda huwo na kurikodi kazi nzuri tungeendelea kuwazungumzia mpaka leo kwa matunda mazuri wangepata.
Wasanii wa Burundifleva wajifunze kupendana na kuangalia agency za wenzao sio kwa lengo lakusema nani ni mkali au nani ni wa kwanza, kwa nia hiyo hawatakuza sana yao.
Msanii mwenye Busara na aliyekuwa na lengo la kujitangaza kimataifa, hata siku moja hajawahi kufikiria kwamba nimfunike msanii fulani au awe on top, bali anafanya kwa kadri ya uwezo wake, kuwa tofauti, mengine anawaachia watazamaji au mashabiki.
Tuwakumbushe wasanii wa Burundifleva kuwa msisahau mlipotoka na tizameni nchi jirani zinazidi kuwaacha kimuziki wakati mnavipaji ila zingatieni kuwa Umoja ni Nguvu Utengano ni Udhaifu hakuna aliyebora kati yetu wote tunaudhaifu wetu.