Ni kweli kwamba striking maker wa wimbo Ile Ile, Magic Soldier maarufu kama Kingorongoro anatarajia kuachia wimbo wake mpya wiki hii aliyomshirikisha mkali wa Burundifleva King Sabbatum B.
Hivi karibuni kumekuwa na stori za kupishana na kauli za mashabiki wa wasanii hawo wawili, chanzo ni taarifa zilizodai kutoka kwa wapenzi wa muziki nchini kwamba Sabbatum B ndie kamuomba rapa Magic soldier collabo huku wengine wakisema kuwa Magic Soldier ndie kampigia simu mke wa Sabbatum B ili amufikishie ombi lake la kushirikiana na mmewe.
Africanmishe ilijitaidi kutafuta ukweli kuhusu nshu hii, imedhiririka kuwa hakuna aliye mpigia simu mwingine au kumuomba mwingine bali ni maelewano kutoka pande zote mbili na projection yao hii ni ya tangu zamani ila walitafuta mda muafaka wa kukamilisha lengo yao na wameana inawabidi mwaka huu 2017 watimize kazi kubwa kwasababu wote wawili wamekwisha tambua ni jinsi gani wataiteka soko la muziki na kujitambulisha kimataifa zaidi kupitia collabo yao.
Magic Soldier aliwaomba mashabiki zao wakae mkao wa kula kwa kusubiria ujio mpya wa wimbo wao mpya mwishoni mwa wiki hii.