Download Mp3 from African

Mfanyabiashara Mwanza mbaroni kwa tuhuma za dawa za kulevya.





Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mfanyabiashara wa vipuri vya magari jijini mwanza kassim Hemed hamad kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya heroine kiasi cha pinchi 240.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Naibu Kamishna wa polisi Ahmed Msangi amesema Kassim ambaye ni mkazi wa Kanyerere kata ya Butimba amekamatwa majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo, akiwa na dawa hizo nyumbani kwake baada ya polisi kupewa taarifa na raia wema kwamba mtuhumiwa huyo ameingiza mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya kutoka jijini Dar es Salaam.

Aidha kamanda huyo wa polisi mkoani Mwanza DCP Ahmed Msangi ameongeza kuwa Jeshi la polisi limewatia mbaroni watuhumiwa wengine xi wakiwa na dawa za kulevya aina ya mirungi, misokoto ya bangi na kete za madawa ya kulevya katika msako uliofanyika kwenye wilaya za ilemela na nyamagana Jumatano wiki hii.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza anatoa rai kwa wakazi wa jiji la Mwanza kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini mtandao wa watu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ndani na nje ya mkoa, huku akisema Jeshi la polisi halitamuonea haya mtu yeyote katika vita hiyo.





Tag : lainnya
Back To Top