Msanii BienFrima anayetamba na wimbo wake Uko Wapi, amesema kuwa hana bifu na kundi nzima la Masodja Yeroo kama jinsi wanavyo zungumza mashabiki na baadhi ya watangazaji pia alisisitiza kuwa haitaji wala hataraji kuwa na bifu na msanii wowote kwani hiyo itafanya kushusha mziki wake.
Hivi karibuni BienFrima alisikika kwenye gazeti la Mishe Mishe Media na kusema kuwa inabidi watu wajipange pindi wanapofanya interview ao wanapotaka kumzungumzia mtu na sio kukurupuka tu, akaendelea kwa kusema kuwa watu wasiwe na shepu ya kike.
Haya yote Mkali wa Uko Wapi aliyasema ni kutokana na homa ya bifu inazidi kuitawala muziki wa Burundifleva huku wakifikiria ni njia nzuri ya kujitangaza kimataifa, kumbe wanazidi kutangaza ujinga pasipo kujuwa.