Download Mp3 from African

nelly Nat afunguka kuhusu ziara yake nchini tanzania

Mtangazaji wa kike wa kituo cha Redio Rema FM ya Burundi, Nelly Nat aliwasili leo hii nchini  Tanzania katika ziara yake ya kikazi zaidi kama mtangazaji.

Baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege  nchini Tanzania, mvua ya maoni ilianza kumwangika, wasomaji wengi wa african Mishe  wakaonyesha kutamani kumfahamu zaidi mtangazaji Nelly na kwanini amechagua Tanzania kwa ziara yake ya kwanza kama mtangazaji.

Nelly Nat alitufungukia zaidi kuhusu ziara yake nchini Tanzania huku akisema kuwa amekuja kujifunza zaidi wanacho kifanya watangazaji wa Bongo na kujua mengi zaidi siri ya mafanikio ya muziki wa Bongo Fleva, kwasababu tayari anatambua kuwa muziki wa Bongo Fleva imepiga hatua kubwa zaidi kwenye ulimwengu wa muziki. 
Katika maojiano na muandishi wa habari wa Mishe Mishe Media nchini Tanzania, Nelly Nat alifunguka  kuhusu ziara yake nchini Tanzania na kusema 
''kwanza asante kwenu Mishe Mishe media tunaifuatilia vyema  ata nyumbani (Burundi), na pia asante kwa kuniweka karibu na wasikilizaji kwa kufunguka zaidi kuhusu uwepo wangu hapa. Niya ya ziara yangu Tanzania ni kuja kwanza kujifunza zaidi  na kujua namna gani wenzetu wanafanya nini zaidi yetu, ninaimani nitatembelea redio nyingi na kufahamu wanacho kifanya na kupata maujanja  kupitia kazi zao.
Pia nina mpango wakukutana na wasanii tofauti ila zaidi nitafanya maojiano na Q Boy na Lizer Classic wa WCB. Nitajaribu pia kukutana na watangazaji wa Clouds FM na wengine ili tuwe na ushirikiano mzuri kwasababu tunafanya kazi moja inabidi ushirikiano ni walazima sana.'' 

Mwisho alitoa ushauri kwa vijana wanaotaka kuingia kwenye fani ya utangazaji, Nelly Nat alisema  kuwa tayari amekwisha tambua kazi ya utangazaji ni kazi ya kujitolea sana sio kama wanavyo fikiri wengine.

''Wanao taka kuingia kwenye fani hii wanakaribishwa ila sio kazi ya kujaribu na ulelemama ni kazi ya kujitolea maana wengi hufanya wakidhani ni signal ya mtu kupata umaarufu,kama una kipaji follow your dreams na kusoma pia ni muhimu.

Mwisho nawaambia wasikilizaji wangu tuwe pamoja kama kuna mengineyo wanapenda wanifahham zaidi wasijali tutaongea nawo na kupana mawasiliano. Asanteni.''


Back To Top