Vanessa Mdee, Gosby, Mabeste na wengine, walijikuta wakihaha miaka
takriban mitatu iliyopita baada ya kupigwa chini na label ya B’Hits.
Kipindi hicho Vee ndio alikuwa ameanza kupata umaarufu.
“Nilipigwa chini na label, label ilinipiga chini kama kiazi chenye
moto,” Vee alisema kwenye mahojiano na kipindi cha Up Close &
Personal cha K24 ya Kenya.
“Waliniacha kwa sababu ambazo zilikuwa zikijirudia, ulikuwa ni wasaa
mchungu mtamu kwasababu kipindi hicho Closer ilikuwa inafanya vizuri
sana, Me & You ilikuwa inafanya vizuri sana kwahiyo nilihitaji zaidi
na nilikuwa nazo zaidi kwenye studio lakini tuligombana sasa ningeweza
kwenda kuchukua muziki?”
Aliendelea, “Kwahiyo nikasema nahitaji kumpata mtu ambaye anaweza
kupatia sauti yangu. Shout out kwa Hermy kwasababu sasa sisi ni familia,
ni kaka yangu daima. Kwahiyo nilikuwa naijua hii bendi ya Navy Kenzo
toka Arusha na wakati huo walikuwa wakijulikana kama Pah One. Pah One
ikaja kuvunjika na wawili kati yao walikuwa wanataka kwenda nje kusoma
masters, nilienda kwenye studio yao ambayo wakati huo ilikuwa nyumba yao
na nikamuambia Nahreel ‘nakuaminia, nadhani mimi na wewe tunaweza
kufanya mambo makubwa pamoja.’
“Muda huu Nahreel alikuwa tayari kufungasha virago na kuondoka
‘nimechoka na mambo haya ya muziki.’ Na nikamuambia, acha tufanye kazi
na nikamuambia ‘nichezee nyimbo zako’ pamoja tulielewana sana na imekuwa
ni even out tangu hapo na ninajivunia sana Navy Kenzo na Nahreel ni genius
na ndiye mtayarishaji mkuu wa album yangu.”

Tag :
lainnya