Download Mp3 from African

RAIS WA SUDAN KUSINI ATAKA WANAOBAKA WANAWAKE KUPIGWA RISASI

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir ametoa maagizo kwa vyombo vya usalama nchini humo kumpa taarifa kuhusu matukio ya ubakaji kila yanapotokea ili serikali iwachukulie hatua thabiti wahusika wa matuio hayo.Kiir aliyasema hayo wakati akihutubia wananchi katika mkoa wa Yei na kusema kuwa serikali haipo tayari kuwavumilia watu wanaowatendea wanawake vitendo hivyo na atakaebainika kumbaka mwanamke yoyote basi hatasita kuamuru apigwe risasi.
“Wote ambao wanavunja vifungu vya sheria kwa kuwabaka wanawake na waischana hiyo sio sera ya serikali yetu … mwili wa mwanamke hautakiwi kutumiwa kwa nguvu,” alisema Kiir na kuongeza.
“Nataka Mkuu wa Majeshi, Paul Malong na Waziri wa Ulinzi kunipa taarifa kuhusu kila jambo linapotokea linalohusiana na hili (ubakaji). Katika kesi kama hiyo, tutampiga risasi mtu ambaye amehusika na tukio hilo
Tag : lainnya
Back To Top