Msanii King Moses wa Republic of Burundi Flava mwenye makazi yake nchini Marekani (USA), anatarajia kufanya kazi ya ziada kwenye tasnia ya muziki mwaka huu 2017 kama alivyotufungukia.
Msanii mahiri King Moses, wengi wanapenda kujiuliza maswali kuwa hicho kipaji na hasa sauti anavyoipangilia tena bila kuchoka, je amesomea shule ama kazaliwa nacho? najua anavyowachanganya mashabiki zake ni namna anavyoweza kuimba na akiimba anarudi kutoa kapani katika kunegua, huwezi mfananisha na msanii wowote wala huwezi kusema ali re-create kwa fulani.
Akizungumza na AfricanMishe, King Moses aliweka wazi mipango yake na kusema kuwa mwaka huu 2017 anatarajia kufanya kazi ya ziada kwa lengo la kijitangaza kimataifa zaidi na kuongeza kuwa alikuwa kimya siku chache kwa kutazama namna gani ya kutoka na kuwaacha mbali.
Aidha King Moses anatarajia kuachia wimbo ambao utakuja na video baada ya kuona kuwa njia pekee ya kujitangaza kimataifa ni kufanya jinsi wanavyo fanya wengine na kuzidi kuja tofauti na awali.
Tusubiri ujio mpya wa wimbo wake atakama hajasema wimbo huo utatoka lini lakini dalili zinaonesha kuwa unaweza ukaachiwa mwezi ujao na kazi nyingine nyingi zitafuata,