![]() |
Hakizimana Cecile |
Nancy na Hakizimana Cecile ni kati ya waigizaji wa kike warembo wa hapa Burundi, wote wanazidi kufanya vizuri kwenye ulimwengu wa filamu. Nancy na Hakizimana Cecile wanafanya pic na vigumu kujua nani zaidi katika uigizaji wa pic sababu kila mtu anasababu yake ya kumkubali mmoja wao.
Tukienda kwenye fashion Nancy na Cecile wote ni wakali pia ni warembo katika swala la uvaaji, na tukienda kwenye ujasirimali Nancy na Cecile hawapo nyuma.
Tulijaribu kuwatafuta warembo hawa, tulifanikisha kuojiana na Hakizimana cecile kutoka kwenye kundi la TambweThe Great Film, na alitufungukia kuhusu swala nani zaidi kati yake na Nancy huku akijidai kuwa bila shaka anajikubali labda mwingine ni namba mbili kwenye tasnia ya filamu nchini Burundi.
![]() |
Nancy |
Mrembo Cecile alisema: "Mwigizaji huwa anapimwa na kuamuliwa na watazamaji kama anafaa au hafai kuigiza wahisika fulani katika michezo, na uamuzi huo unatolewa baada ya wao kutazama michezo miwili mitatu tu aliyoigiza. Bila shaka kila mwigizaji ana sifa zake za kuigiza mtu wa aina fulani, lakini anataka awe na uhodari wa kuigiza kila aina ya watu, na akipata nafasi ya kuigiza mtu wa aina tofauti na yeye mwenyewe nadhani hakika atapenda kujaribu. mimi sifa hizi zote ninazo, haina aja yakutafuta nani zaidi kati yangu na yule( Nancy) labda atakuwa namba mbili yangu ."
Ingawa Nancy ni muigizaji anayejulikana na watu wengi nchini, Cecile alijibu nakusema kuwa ''yule anatengenezwa ila atambuwe kuwa lengo langu ni kujitangaza kimataifa zaidi na wasubiri filamu yangu mpya inakuja inaitwa Chozi hapo ndipo wataamini kuwa mi ni zaidi yao ila sio kama namdharau bali namkubali kwasababu anajitahidi kuigiza vizuri.''
Je unataka kutambua alichojibu Nancy baada ya taarifa hii? endelea kufuatilia Africanmishe.