Straika wa Yanga, Amissi Tambwe mwenye mabao saba, ameibuka na kusema kuwa, alikuwa na presha kuona wapinzani wao Simba wamewazidi pointi nyingi, lakini sasa presha yake imeshuka.
Awali, Simba ilikuwa juu ya Yanga kwa pointi nane, lakini mzunguko wa kwanza umemalizika wakiwa kwa tofauti ya pointi mbili.
Tambwe alisema mzunguko wa kwanza ulikuwa mgumu kiasi cha kuwachanganya zaidi kufuatia kupishana pointi nyingi na wapinzani wao, lakini wamepata faraja kufuatia wapinzani wao hao kupoteza michezo miwili mwishoni.
“Mzunguko wa kwanza ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na ulikuwa mgumu sana kutokana na wapinzani wetu kutupita pointi nyingi zilizotufanya tupigane kufa na kupona hadi hapo tulipofikia.
“Lakini tunashukuru Mungu kuona tumewasogelea na kubakiza pointi mbili tu ila sasa hivi afadhali naweza kutembea kwa furaha,” alisema Tambwe.
Tag :
lainnya