Download Mp3 from African

SPORT EXTRA: Rashidi Leon ni mmoja wa beki bora wa kushoto kwenye Primus League

Mchezaji wa timu ya taifa Intamba Murugamba wa LLB nchini Burundi, Rashidi Leon akiwa nahodha wa klabu hiyo bila shaka ndie anazidi kuonekana beki mahiri wa kushoto kwenye Primus League msimu huu wa 2016/2017.

Beki wa kushoto ambae anazidi kushangaza watu kwa jinsi anavyo pangwa kwenye kikosi cha timu ya taifa akicheza kama beki wa kulia wakati katika timu yake anazidi kushamiri kama beki wa kushoto.

Rashidi Leon anazidi kuwagaragaza wachezaji walionekana bora miaka za nyuma, kwasababu ana mbio, chenga na uwezo wa kusaidia mashambulizi. Pia ni mkakamavu na sio mbishi, kitu ambacho kinamfanya kumtofautisha na mabeki wengine wa kushoto. Beki huyu wa LLB  anastahili kuwemo kwenye kikosi cha timu yoyote hile.
Beki wa kushoto huyu, amekwisha ichezea sana LLB na timu ya taifa katika mechi za kimataifa (CHAN, Cecafa...).
Ni beki mahiri wa kushoto kutokana na kazi kubwa anayoifanya, ana uwezo mkubwa wa kupandisha mashambulizi, kupiga krosi, kufunga na pia kuwazuia mawinga machachari.
Ameifanya LLB kuwa moja ya timu ngumu kufungika msimu huu, lakini pia hajawahi kukosekana kwenye kikosi cha timu ya taifa.





Back To Top