Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam, Rais Magufuli amesema hawezi kuzungumza lolote kuhusu muswada huo kwa kuwa muswada huyo utajadiliwa bungeni na wabunge wote.
“Kuniambia mambo ya bunge ambayo bado sijaletewa, utakuwa unanionea katika utawala wa bunge,” Magufuli alimjibu mwandishi aliyehoji kuhusu muswada huo. “Tuwaache wabunge watimize wajibu wao. Sasa unaponiambia ukiletwa niikatae nataka nikueleze bila unafiki siku utakapo fika siku hiyo hiyo nitausaini, ili msubiri kama utakuja wakati mwingine mje muubadilishe, sitaki kufrastuate mambo ya bunge,”
Aliongeza, “Lakini lazima tukubali kwamba hii sheria imechelewa, na unakuta mnazungumza kwa lugha ya wamiliki fulani fulani. Lakini muswada huu sifahamu wabunge watakacho amua lakini niya ni kulinda waandishi wa habari,”
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii ili wapate kipato kutokana na kazi wanazofanya.
“Tanzania ni tajiri, kinachotakiwa ni namna ya kubalance rasilimali, katika kufanya hilo mimi nimeamua kubana matumizi serikalini kwa mfano nimedhibiti safari za nje kwa kuanza na mimi mwenyewe, tangu niingie madarakani nimepata mialiko 47 lakini nimekwenda mialiko mitatu.” Alisema Rais Magufuli.
Tag :
lainnya