Download Mp3 from African

BREAKING NEWS: Bweni lateketea kwa moto shule ya ufundi Mtwara.

Bweni la shule ya ufundi mtwara la taketea kwa moto, ambapo chanzo cha moto huo imetokana na italafu ya umeme ambao upo katika bweni hilo. Bweni hilo  ambalo lilikuwa likitumiwa na wasichana katika malazi.

"Bweni limeanza kuwaka moto asubuhi ya leo ambapo ndani ya bweni hili hakukuwa na mtu ndani kwani shule ilikwisha fugwa tangu mwezi ulipita tangu tarehe 28 hivyo hakukuwa na wanafaunzi ambao walikuwepo katika bweni hili, ila wapo baadhi ya walimu ambao walikuwa wanalala katika bweni hili ambao wamekuja kwa ajili ya kusahisha mitihani" alisikika shuhuda mmoja ambaye alijitambuliasha kwa jina Juma ambaye ni mwanafunzi wa katika shule hii.Aidha kikosi cha ukoaji cha zima moto kiliwasili katika eneo la tukio ikishirikiana na kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ili kuweza kuuzima moto huo, kwani moto alikuwa ni mkubwa ukilinganisha na ukubwa wa bweni.

Kwa taarifa za awali hakuna maafa ya kifo ambayo yamesababishwa na moto huo zaidi moto huo kutekeza vitu vilivyokuwepo ndani ya bweni hilo.
Tag : lainnya
Back To Top