Download Mp3 from African

CAN 2017: Habari mbaya inaendelea kwa DR Congo

Baada ya Yannick Bolasie kujeruhiwa katika Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester United na atakuwa nje ya uwanja miezi nne, kwa tarifa hiyo mchezaji nyota wa DR Congo hataudhuria Kombe la Afrika.

Habari nyingine ya mchezaji mwingine muhimu, Padou Bompunga atakosa pia Kombe la Afrika Can2017, mchezaji wa katikati wa AS Vita Club alilazimika kujiondoa baada ya kujeruhiwa Jumapili katika mechi dhidi ya FC Renaissance.

Padou Bompunga analazimika kupewa mapumziko ya miezi miwili baadae ndio atapewa kibali chakurudi uwanjani. 
Kiungo huyo wa miaka 24, alijeruhiwa kwenye mguu wake wa kulia na ushiriki wake katika CAN 2017 itakayoanza rasmi kuanzia Januari 14- Februari 05 nchini Gabon, ni kama tayari ametengwa.


Kumbuka kuwa DR Congo ilipangwa katika Kundi C pamoja na Ivory Coast, Kingdom of Morocco na Togo.

Tag : Michezo
Back To Top