Download Mp3 from African

Mtayarishaji wa muziki wa bongo Hermy B anasema Producers wa bongo wengi masikini

Mtayarishaji wa muziki na mmiliki wa studio ya 'B Hits' Hermy B amefunguka na kusema kuwa watayarishaji wengi wa muziki nchini Tanzania ni masikini na maisha yao hayafanani kabisaa na majina yao.
Hermy B amesema hayo kupitia concern human relationship yake ya twitter na kudai kuwa watayarishaji wengi wa muziki wa bongo hawana tofauti na watu wanaobeba mizigo (Makuli) kwani wanafanya kazi kubwa sana lakini kipato wanachopata kutokana na kazi hiyo ni kidogo mno kiasi cha wengi kuwa na maisha ya chini ukilinganisha na majina yao.
"Producer Wa muziki Tanzania hana tofauti na kuli anayebeba mizigo bandarini...anatumia nguvu nyingi lakini kipato hafifu...wengi ni maskini" aliandika Hermy B
Lakini mbali na hilo Hermy B alisema kuwa hana uhakika kama baadhi ya wasanii wa bongo wanakumbuka kufanya Investement ili kuzidi kujiongezea kipato kutokana na pesa ambazo wamekuwa wakipata kupitia muziki wao na dili za hapa na pale.
"Nahisi wanamuziki wa kibongo wanamiliki nguo nyingi kuliko vitega uchumi" alisema Hermy B
Tag : lainnya
Back To Top