Download Mp3 from African

Rais Dkt John Pombe Magufuli ameandika historia kwa wananchi

 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na bodi hiyo ,aliyepo kulia kwake ni katibu tawala wa mkoa wa Arusha  Richard Kitweka,aliyepo mkono wa kushoto kwake ni mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema ,wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha
 Wajumbe wa bodi ya barabara ya Mkoa wa Arusha waliohudhulia kikao cha 38 cha bodi hicho,jijini Arusha.
 
Rais Dkt John Pombe Magufuli ameandika historia kwa wananchi tangu Tanzania ipate uhuru na kuelekea kutimize mwaka ane madarakani kwa kuipatia Wilaya ya Ngorongoro  barabara ya lami yenye urefu wa kilomita sixty tangu Wilaya hiyo ianzishwe.


Haya yameelezwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakati wa Kikao cha 38 cha bodi ya barabara cha Mkoa huo.


Gambo alisema  barabara hiyo inayotarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami  na itaunganisha  mji wa Wasso hadi Sale kilomita sixty imepata Baraka zote kutoka kwa Rais Magufuli.


Gambo ameeleza katika Kikao  hicho kwamba  Rais Magufuli ameagiza kuanza kujengwa kwa barabara hiyo mara moja  kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi wakati wa Kampeni alipokuwa katika Wilaya hiyo.


Amesema barabara hiyo  inatarajiwa kutekelezwa na Wakala wa barabara mkoani Arusha ( TANROADS).


Mkuu huyo wa Mkoa amesema  hii ni hatua muhimu sana kwa Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro ,Wilaya  haina hata barabara moja yenye kiwango cha lami.


Mkuu huyo wa Mkoa pia alisema  fedha zinazotolewa na wafadhili benki ya dunia  sio msaada  bali ni fedha za mkopo kwa Tanzania ambazo  Tanzania italazimika kuzilipa hapo baadaye.


Akitoa shukrani zake mbunge wa jimbo la Ngorongoro Tate William Ole Nasha alisema kwa mala ya kwanza Ngorongoro inapata barabara yenye kiwango cha lami, kweli itakuwa furaha kubwa sana kwa wananchi wa Wilaya hito.


Wilaya ya Ngorongoro ni kati ya Wilaya sita za Mkoa wa Arusha  ambapo Wilaya hii inakabiliwa na matatizo makubwa ya miundo mbinu ya ukosefu wa barabara za uhakika ambapo usafiri katika Wilaya hiyo ni wa kubahatisha kutokana na kukosekana kwa miundo mbinu ya uhakika ya barabara kwenda maeneo ya vijijini.


Hivi sasa TANROADS inahudumia kiasi cha kilomita 1,220 katika Wilaya   za Mkoa wa Arusha zikiwemo  barabara kuu na barabara za Mkoa alisema Meneja wa Mkoa Mhandisi  John Kalupale.

Picha ya Pili
Wajumbe wa bodi ya barabara ya Mkoa wa Arusha waliohudhulia kikao cha 38 cha bodi hio,jijini Arusha
Tag : lainnya
Back To Top