Timu ya AS Inter Star imeitambia Messagé Ngozi kwa mabao 2-1 dhidi ya Messagé Ngozi , jana Jumamossi kwenye Uwanja wa Mwana Mfalme Prince Louis Rwagasore.
Mechi imekuwa ya kupendeza sana huku timu ya kutoka mkoani Ngozi imeonekana ikimiliki mpira sana kama kawaida ya timu hiyo ila mwishowe wamepatwa na mshangaho kuona mechi imemalizika kwa ushindi wa timu ya mjini Bujumbura Inter Star kupitia mchezaji kongwe wa timu hiyo ajulikanaye kwajina la Puchu de Guerre ambae ameingia kipindi chapili na kuleta mabadiliko makubwa huku akifanikiwa kuona lango dakika ya mwisho kwa kuizawadia timu yake ushindi.
Tuwakumbushe kuwa Messagé Ngozi ina pointi tatu tu katika mechi tatu baada ya kuifunga Vitalo bao 1-0 katika mechi ya kwanza huku mechi mbili imepoteza kwa matokeo isiyo ridhisha ya tatu bila ikiwa nyumbani kwake Ngozi dhidi ya Atletico Olympic pia na jana 2-1 dhidi ya Inter Star.
kwasasa timu ya As Inter star inazidi kuongoza baada ya kufanya vizuri mechi tatu ikiwa na pointi zote tisa na kuwa kileleni sambamba na LLb Academic.
Katika wiki ya tatu ya Ligi Kuu Primus League, LLb imepata ushindi wake kwa shiai wa bao 1-0 dhidi ya Muzinga, Flambeau De l'Est ya Ruyigi imefanya vizuri ugenini na kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Buja City kupitia mchezaji wake nyota ajulikanae kwajina la Dubien pia Les Lierres imeridhika kwenda sare ya 1-1 dhidi ya Messagé Bujumbura. Mechi zingine zitaendelea leo na matokeo bila shaka mtazipa hapa.
Picha chache za Inter Star 2-1 Messagé Ngozi