Leo Ijumaa tarehe 02/ 12/2016 msanii Dj Pro Negger amewasili nchini mwake Republic of Burundi akitokea Afrika Kusini, msanii huyo anayetamba na ngoma yake ''Maisha Na Muziki'', alipokelewa na mashabiki zake pamoja na watangazaji wa habari pia na familia yake kwa shangwe na furaha.
Katika maojiano na waaandishi wa habari Dj pro alifunguka kuhusu present yake ijulikanayo kwajina la White Party tarehe 17 Decemba, 2016 pande za Havana Night Club.
Msanii huyo alifurahishwa na mapokezi ya mashabiki zake kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura na kusema kuwa anatarajia kuachia nyimbo na video yake mpya siku hivi karibuni,
dah ninafura sana siku ya leo kukutana na wadungu zangu, na kuona maandalizi kama haya ni kitu hakijawahi kunifikia tangu nianze kazi ya muziki. Na maandalizi yapo mengi kwanza nimekuwa natarajia kuachia nyimbo mpya na baadae ya hiyo nilikua natarajia kuachia video mpya kwasasa nipo kwenye arakatia ya kuachia video na nyimbo mpya kwa pamoja.
Kuhusu kiingili ghali kuliko present za wasani wengine, Dj pro alijibu nakusema kuwa lazima twende na wakati tusiwe na tabia ya kujizarau.
Baadhi ya watu wanapenda kujizarau sana yaani wanafanya kitu bila kujiamini, tizama awali wasanii kutoka Nigeria wanakuja hapa wanafanya present za elfu thalathini, kwanini na sisi tusifanye. Endapo unataka kufanya kazi na diamond ao msanii wowote mkubwa na ungali unafanya present ya elfu moja, hauwezi ukafaulu ila ukijiamini kufanya present kubwa ninaimani utafikia malengo.
Kuhusu usalama wa nchi na kwanini alichukuwa wasanii wa kusini kwenye White Party yake kuliko wasanii kutoka sehemu nyingine, msanii huyo alifunguka na kusema kuwa anapenda kufanya kazi na watu wanao penda kazi zao kwanza,
kuna watu wanafanya muziki kwa malengo tofauti, ili apate mademu na kuna wengine wanafanya muziki ili wafanikishe ndoto ya kuwa na maisha mazuri kupitia kazi ya muziki ndio maana mi nafanya kazi na watu wanao penda kazi, kwa namna hiyo sasa naanza kuingia kwenye tuzo kubwa kubwa za dunia na kuhusu usalama wa nchi naona kwamba Republic of Burundi amani ipo kabisa tumezunguuka sehemu nyingi nimeshuhudia kama amani ipo na watu wamejifunza mengi tofauti na awali.
Msanii Dj pro kutoka Burundia anayetamba na kibao Maisha na Muziki, alisema hatawaangusha mashabiki zake kwenye White Party siku hiyo na kuongeza kuwa kuna surprise nyingi sana kwajili ya watakao pata bahati ya kufika siku hiyo.