Baadhi ya nyumba zimebomoka na kujeruhi watu. Hakuna taarifa rasmi ya kutokea kwa vifo.
“Nimelishuhudia Misungwi hatari nyumba inatikisika unaona kabisa .. Tuzidisheni ibada jamani,” ameandika mwananchi mmoja kwenye Facebook.“Mwanza tumehaha, tetemeko limenikuta nipo ndani nakula, tukawa tumetoka nje ili kupisha tusije kudondokewa na nyumba, ile tetemeko limeisha tukarudi ndani, ile tunarudi ndani tetemeko likaanza tena. Lakini tunamshukuru Mungu kwetu limepita salama, pole kwa waliopatwa na maafa,” ameandika mwingine.
“Limedumu kwa muda wa zaidi ya dakika tatu huku Simiyu mwishowe lilimalizia kwa kishindo watu wametaharuki sana,” ameandika mwananchi mwingine.
Tetemeko hilo limesababisha taharuki kubwa kwa wakazi wa maeneo ya Mwanza na Kagera. Hizi ni picha zaidi za nyumba zilizoathirika.
“Daaaaa!!ilikuwa ni shiida yaan tetemeko hili cjawahi kushuhudia limekaa muda mrefu kwel yaan nilikuwa nimelala nyumba ilivyotingishika had kitanda kikawa kinahama toka sehem moja kwenda nyingine Mungu baba nakuomba hii hali isirudie tena baba,” ameandika mkazi wa Mwanza, Boniface Shayo.
Tag :
lainnya