Msanii pia Muigizaji wa filamu kutoka Tanzania, Hemed Suleiman almaarufu kama PHD, aliwasili kwa mara ya kwanza nchini Republic of Burundi jioni kwenye uwanja mkuu wa Bujumbura akipokelewa na kundi nzima la waigizaji wa filamu nchini ijulikanayo kama The Brothers.
Mapokezi imekuwa ya kupendeza huku mashabiki zake wakimpokea kwa shangwe na furaha, Msanii pia Muigizaji huyo ameitishwa na kundi la The Brothers kwa kukamilisha filamu yawo ''Burundiano inward Dar'' aliyo shirikishwa na kundi hiyo pia kwa tamasha itakayo fanyika Decemba , 04 ,2016 kwenye ukumbi wa La Coast Beach.
Baadae msanii huyo na kamati nzima ya The Brothers iliandaa maojiano na waandishi wa habari usiku huku msanii huyo akijaribu kujibu baadhi ya swali ya waandishi wa habari walio udhuria sehemu hiyo.
Tazama maojiano ya PHD na waandishi wa habari nchini Republic of Burundi hapa