Katika arakati ya kuandaa msimu mpya ambayo itaanza hapo mwezi Septemba mwaka huu 2016. Klabu nyingi za daraja la kwanza nchini Republic of Burundi zimeanza kuandaa vizuri uku baadhi ya timu zikijielekeza nje ya nchi na zingine zinazidi kutafuta wachezaji.
Kocha Mkuu wa LLB Academic ya Bujumbura amefunga kuusu msimu mpya utakao anza ivi karibuni na amewahaidi mashabiki wa klabu hiyo mambo makubwa tofauti na msimu uliyo pita.
"ya unaona gisi tunaendelea na mazoezi na tumejaribu kusajili wachezaji wengine ili kujitayarisha vilivyo na kama unavyo fahamu hii timu Lydia Lidic ni timu imezowea kutoka nafasi ya kwanza ao ya pili ila mwaka jana tumeambulia nafasi ya tano na tumestahili nafasi hiyo kwasababu ya maandalizi mabovu. ila kwasasa tumeongezea nguvu ili tuangalie kama tunaweza kurejesha sifa zetu." amesema kocha Maele.
Kocha Mkuu wa LLb Academic amekuwa wazi na kutaja wachezaji ambao amesajili msimuu huu uku akiwa na imani kwamba wachezaji hawo watamsaidia kwenye Ligi Kuu na katika kombe la Raisi.
"wachezaji waliokuwa mwaka jana ningali naho, kuna wachezaji ambao ni meongezea ni pamoja Tambwe Floribert, Kaya; Rugo wakitokea katika timu ya Vitalo, Abdoul ambaye amewahi kuwa mchezaji wetu mwaka juzi ila ametokea Zanzibar na amekuwa nacheza uko, golikipa Mutombo pia na Celestin na tunawachezaji wapya vijana."
Kuusu lengo lake msimu huu itaanza ivi karibuni, kocha Maele ameifungukia Mishe Mishe na kusema
"lengo yetu ni kutoka wa kwanza ao wa pili labda Mungu apanguwe ila Mungu akisaidia kutokana na maandalizi tunayo kwasababu maandalizi mazuri ndiyo mafanikio. kitu ambacho naweza waambia mashabiki wa LLb waache kusikia maneno ya watu, kwanza naishukuru FFB kwa kupatia kila timu milioni kumi ya kusajili wachezaji na milioni sita ya maandalizi za mechi za mikoani. sasa ukiwa na milioni kumi utashindwa kusajili wachezaji?. Wengi wanasema kwmba Mzungu ameitoka LLB na mengi mengi ila watambuwe kuwa Mzungu nimeongea naye na angali kwetu. kitu cha muhimu nawahaidi msimu huu nitofauti na mwaka uliyo pita."
Tayari timu hii imekwisha cheza mechi ya kirafiki na mechi zake zote zinaonekana kama ni timu inakuja kuleta upinzani mkubwa katika Ligi Kuu ya Primus League,
