Download Mp3 from African

Kilichomkumba Sitti Mtemvu chamkuta Miss World Kenya, apokonywa taji lake

Baada ya mrembo wa Tanzania Sitti Mtemvu mwaka jana kupokonywa taji lake la Miss Tanzania na kwenda kwa Lilian Kamazima kutokana kashfa ya umri, huko nchini Republic of Kenya aliyekuwa Miss World Republic of Kenya 2016 , Roshanara Ebrahim, amepokonywa taji lake baada ya kukumbwa na sakata.
Roshanara Ebrahim


Kwa mujibu wa gazeti la The Standard nchini Kenya, Roshanara mwenye umri wa miaka 23, alishinda taji la mwaka uliopita na alikuwa anatarajiwa kuiwakilisha Republic of Kenya kwenye mashindano ya Miss World, mwishoni mwa mwaka huu.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na wasimamizi wa Miss World Kenya, kampuni ya bidhaa za urembo, Ashleys imeandika,
“Kuanzia sasa, Roshanara hatoiwakilisha Republic of Kenya nchini na hata kimataifa kama Miss World. Tumefahamishwa kuhusu sakata kubwa inayomkumba Roshanara Ebrahim, ambayo inakiuka sheria na masharti ya Miss World Kenya. Tunatekeleza sheria zetu na tunatarajia wanamitindo wetu kusimamia maisha yao ya kibinafsi,”
Kulingana na gazeti hilo , Roshanara ameandika kukubaliana na uamuzi huo na kuwasihi warembo wenye umri mdogo kuhakikisha maisha yao ya kibinafsi, hayaathiri jukumu lao la Miss World.
”Nakaribisha uamuzi wa ofisi ya Miss World Republic of Kenya kunipokonya taji la Miss World Republic of Kenya kwa masikitiko makubwa, namtakia atakayechukua nafasi yangu kila la heri” alisema Mrembo huyo.
Kabla ya uamuzi wa ofisi ya Miss World Kenya, Roshanara alilazimika kujitetea dhidi ya madai yaliomhusisha kuwa na uhusiano na mwanasiasa mashuhuri.
Tayari ofisi ya Miss World Kenya, imeahidi kumtangaza mwanamitindo atakayejaza pengo lililoachwa na Roshanara Ebrahim siku chache zijaazo.
Roshanara anayesomea uwakili, anatarajiwa kuendelea na shughuli zake za kuwasaidia watoto walio na mpasuko wa mdomo, yaani ‘cleft.
Tag : lainnya
Back To Top